Malipo ya Mapema ya 2UP kwa Kombe la Dunia

Kombe la Dunia la FIFA ndiyo jukwaa kubwa zaidi la soka duniani, na sasa unaweza kusherehekea ushindi wako hata kabla ya filimbi ya mwisho.

Kupitia promosheni ya Malipo ya Mapema ya 2UP ya Betika, ikiwa timu uliyoichagua itaongoza kwa mabao mawili (2) wakati wowote katika mechi yoyote ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, bashiri yako italipwa kama mshindi.

Promosheni hii inapatikana kwa:

  • Promosheni hii inapatikana kwa:
  • Bashiri ya mechi zaidi ya moja (Accumulator Bet)

Huhitaji kujisajili kwenye promosheni hii. Weka mkeka wako na ufurahie mchezo.

Jinsi Inavyofanya Kazi

  • Weka bashiri kwenye soko la 1X2 kwa mechi yoyote ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.
  • Promosheni inatumika kwa Bashiri ya mechi moja na Bashiri ya mechi zaidi ya moja.
  • Chagua Timu ya Kwanza (Team 1) au Timu ya Pili (Team 2) kushinda.
  • Ikiwa timu uliyoichagua itaongoza kwa mabao mawili wakati wowote ndani ya muda wa kawaida wa mchezo, uchaguzi wako utastahili Malipo ya Mapema ya 2UP.
  • Mara tu uchaguzi unaostahili utakapolipwa kama mshindi chini ya promosheni hii, matokeo ya mwisho ya mechi hayatabadilisha malipo hayo.

Sheria Muhimu

  • Promosheni hii inatumika kwa mechi zote za Kombe la Dunia la FIFA 2026 pekee.
  • Inatumika kwenye soko la 1X2 pekee.
  • Chaguo la Sare (Draw) halistahili.
  • Inatumika kwa Bashiri ya mechi moja na bashiri ya mechi zaidi ya moja
  • Inatumika kwa bashiri zilizowekwa kabla ya mechi kuanza (Pre-Match Bets) pekee.
  • Ni muda wa kawaida wa mchezo tu (dakika 90 pamoja na muda wa nyongeza wa majeruhi) unaohesabiwa. Muda wa ziada na mikwaju ya penalti hautahesabiwa.
  • Kwa Bashiri ya mechi zaidi ya moja(multi bet), chaguo zilizolipwa kama washindi chini ya promosheni hii zitahesabiwa kama chaguo zilizoshinda ndani ya machaguzi hayo.
  • Bashiri zinazostahili zinaweza zisilipwe mara moja na zinaweza kushughulikiwa ndani ya muda unaofaa baada ya kuthibitishwa kwa matokeo yanayostahili.
  • Bashiri ambazo zimefanyiwa Cash Out kwa ukamilifu au kwa sehemu hazitastahili promosheni hii.
  • Ikiwa mechi itaahirishwa, kusitishwa, au kutangazwa batili, Sheria za Sportsbook za kawaida zitatumika.
  • Betika ina haki ya kurekebisha, kusimamisha au kuondoa promosheni hii wakati wowote kwa uamuzi wake.

Kwa Nini Betika?

Ongoza kwa Mabao 2. Lipwa Mapema.

Pata ushindi wako kabla ya filimbi ya mwisho.

Furahia Kombe la Dunia la FIFA ukiwa na Betika.

Vigezo na Masharti

  • Endapo kutatokea mgogoro wowote kuhusu promosheni hii, uamuzi wa Gaming Board of Tanzania utakuwa wa mwisho na wa lazima kufuatwa.
  • Betika ina haki ya kuwataka washindi kuwasilisha nyaraka za utambulisho na kuthibitisha uhalali wa nyaraka hizo kwa mamlaka husika kabla ya kutoa zawadi yoyote.
  • Betika ina haki ya kutumia majina ya washindi, rekodi za sauti za redio, picha za video na picha za kawaida kwa madhumuni ya matangazo, kampeni za masoko na usimamizi wa promosheni hii.
  • Betika ina haki ya kufuta ushindi wowote na kuchukua hatua stahiki katika mazingira mbalimbali ikiwemo lakini siyo tu:
    • Hitilafu au dosari ya mfumo au programu; au
    • Mashaka ya kuwepo kwa Shughuli Zilizopigwa Marufuku (kama zilivyoainishwa katika Masharti na Vigezo vya Jumla vya Betika).
  • Betika haitoi dhamana kwamba promosheni hii itapatikana kwenye vifaa au njia zote za matumizi, wala kwamba itapatikana wakati wote.
  • Masharti ya promosheni hii yanaweza kufutwa, kuahirishwa au kurekebishwa na Betika wakati wowote.
  • Endapo kutakuwa na Shughuli Zilizopigwa Marufuku, Betika inaweza kuchukua hatua itakazoona zinafaa kulingana na mazingira husika, ikiwemo: Kufuta ushindi au miamala yoyote; Kusimamisha akaunti; Kuweka vikwazo vya kutoa fedha; na/au Kuzuia anwani za IP husika.
  • Promosheni hii inatolewa kama ilivyo bila dhamana yoyote ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayodokezwa kisheria, ikiwemo usahihi wa taarifa, usahihi wa tafsiri, upatikanaji wa huduma, muda wa upatikanaji, ubora wa huduma au kufaa kwa matumizi maalum, isipokuwa dhamana zinazolindwa na sheria zinazotumika chini ya Masharti na Vigezo vya Jumla na Sera ya Faragha ya Betika.
  • Promosheni hii inatawaliwa na Masharti na Vigezo vya Jumla vya Betika (pamoja na sera zote zinazohusika) zilizopo hapa . Endapo kutakuwa na mgongano kati ya masharti haya na Masharti na Vigezo vya Jumla vya Betika, Masharti na Vigezo vya Jumla yatapewa kipaumbele.