MASHARTI YA JUMLA YA MICHEZO YA VIRTUALS
Utangulizi
- Hii ni michezo ya virtual inayomruhusu mtumiaji kuweka dau kwenye michezo mbalimbali ya virtual ikiwemo ligi za mpira wa miguu, michezo ya namba, mbio, na michezo mbalimbali ya 'crash'.
- Wachezaji wote wanaoweka dau kwenye mechi sawa za virtual wataona matokeo sawa.
- Mechi zote za virtual hutengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa Teknolojia ya Sanaa ya Bandia (AI) na mfumo wa nambari nasibu.
- Betika ina haki ya kubatilisha ushindi wowote kwa uamuzi wake pekee na kuchukua hatua zozote za marekebisho endapo kutatokea sababu kama zifuatazo:
- Hitilafu ya mfumo au programu.
- Ukiukaji wa masharti haya au ukiukaji wa Masharti na Vigezo vya Jumla vya Betika.
- Shaka ya shughuli zisizoruhusiwa.
- Endapo shughuli zisizoruhusiwa zitagundulika, Betika inaweza kuchukua hatua yoyote inayoona inafaa ikiwemo kubatilisha ushindi, kusimamisha akaunti, kupunguza utoaji wa pesa, au kuzuia anwani ya IP.
- Iwapo kutakuwa na mgogoro kuhusu bidhaa hii, uamuzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania utakuwa wa mwisho.
- Betika haihakikishi kuwa Michezo ya Virtual itapatikana katika vifaa na njia zote au kuwa itapatikana kila wakati.
- Masharti haya yanaweza kufutwa au kurekebishwa na Betika wakati wowote bila taarifa.
- Betika ina haki ya kuondoa Michezo ya Virtual wakati wowote bila taarifa.
- Kwa kushiriki katika Michezo ya Virtual, wachezaji wanakubaliana na kufuata masharti haya.
- Michezo ya Virtual ya Betika inatolewa "kama ilivyo" bila dhamana ya aina yoyote, iwe ya wazi au ya kudokezwa, isipokuwa zile ambazo haziwezi kuondolewa kisheria kulingana na Sheria za Betika na Sera ya Faragha.
- Masharti haya yanategemea Masharti na Vigezo vya Jumla vya Betika yanayopatikana hapa. Iwapo kutakuwa na tofauti kati ya masharti haya na Masharti ya Jumla, Masharti ya Jumla yatachukua nafasi.
Jinsi ya Kucheza
- Tembelea betika.co.tz na uchague mchezo wa virtual unaopendelea kwenye sehemu ya Virtuals.
- Chagua tukio la virtual linalopatikana.
- Chagua chaguo la dau unalotaka kwa mechi zote zinazopatikana na bonyeza odds ya dau unalotaka kuweka.
- Betslip yenye uchaguzi wako itafunguka, baada ya kufanya chaguo lako, weka kiasi cha dau na bonyeza 'Weka Dau'.
- Baada ya kuthibitisha, dau lako litakuwa limewekwa.
- Ili kuona orodha ya dau zako za Virtual, tembelea betika.co.tz, chagua ‘Virtuals’ na bonyeza alama ya slip (mkeka) juu kulia, pembeni ya Salio. Orodha ya dau zako zote za virtual itakuwepo.
- Michezo ya Golden Race (Keno, Grey Hounds, Horse Race na Instant Games) ina alama maalum ya (?) inayoonyesha mwongozo kamili wa sheria na maelekezo ya mchezo.
Sheria za Kubashir
- Kubashiri kunaruhusiwa kabla muda wa kuanza mchezo wa virtual haujaisha. Chaguo la kubashiri kwa mechi za siku zijazo za tukio husika litaendelea kuwa wazi.
- Endapo mfumo utazalisha ushindi unaozidi kiwango cha juu kilichowekwa, kiasi chochote kinachozidi kitachukuliwa kuwa batili na hakitalipwa.
| Mtoaji | Dau la Chini | Dau la Juu | Ushindi wa Juu kwa Dau | Ushindi wa Juu kwa Siku |
|---|---|---|---|---|
| Golden Race | TZSH 100 | TZSH 1,000,000 | TZSH 10,000,000 | TZSH 20,000,000 |
Masoko ya Soka(Mpira wa Miguu) ya Virtual
- Final Result: Timu ipi itashinda? (1 = Timu ya Nyumbani, X = Sare, 2 = Timu ya Ugenini)
- Double Chance: Kubashiri matokeo mawili kati ya matatu yanayowezekana.
- Halftime/Fulltime: Kubashiri matokeo ya kipindi cha kwanza na mwisho wa mechi.
- Goal Goal/No Goal: Kubashiri kama timu zote zitafunga au la.
- Over/Under: Kubashiri idadi ya magoli kuwa zaidi au chini ya idadi iliyotajwa.
- 1X2+Over/Under: Kubashiri matokeo ya mechi pamoja na idadi ya magoli.
- Total Goals: Kubashiri idadi jumla ya magoli yatakayofungwa kwenye mechi.
- Correct Score: Kubashiri matokeo sahihi ya mwisho ya mechi.
- Multigoal: Kubashiri idadi ya magoli ndani ya kipimo fulani (mfano 0-2).
- Asian Handicap: Kubashiri timu itakayoshinda kwa kuzingatia handicap iliyotolewa kwa timu iliyochaguliwa. (Mfano: -1, ili kushinda bashiri, timu iliyochaguliwa inatakiwa kushinda kwa magoli 2 au zaidi. Ikishinda kwa 1 bashiri itabatilishwa na ikipoteza au kutoa sare, bashiri imeshindwa).